12/01/12 23:23:16.59
Kwa nini ? Uliza swali, kama sote tungekuwa wasomi, matajiri
Ni nani angelifanya kazi za kutisha na hatari mfano ya mochwari
Kila mmoja wetu hapa mjini kaja kwa dili
Kila kitu, kila mahali
Na hata ngozi ya mtu dili
Wengine wachawi, waganga feki
Matapeli, wasafiri kafiri
Wakati wengine wapole kama walokole
Mchana pirika nyingi maofisini
Kumbe night kali, kahaba
Shuga, jambazi, mengine ya kusitiri
Wapo waliopoteza maisha katika kufight life
Kumbukumbu zao zimebaki makaburini
Na wapo waliopoteza kabisa tumaini la kuwini
Hao roho zao utadhani wamezitoa rehani
Wakikutight mahali fulani
Inabidi uwakabidhi mshahara wote wa mwisho wa mwezi
Kweli Bongo kutafuta braza
Utajajuta utakapojikuta huna hata bukta
Shauri yako we tegesha tu kama golikipa
Na hao unaowategemea mwishowe watakutosa
Huna elimu, hun fani
Lakini nguvu, ulimi, uchumi unao unaukalia
Kumbuka
Kupata au kukosa yote ni kawaida
Sometimes unalala unaota unakula
Unakunywa, unapiga denda
Na kula uroda na demu bomba
Ukikurupuka tu unakuta patupu
Hakuna kitu